MOVIE NA VICHEKESHO

Simulizi ya Fred Vunjabei iliyobadirisha Maisha Yangu Kimtazamo

Fred Vunjabei – Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa na duka moja dogo sana Kariakoo (Goli), baada ya kujikusanya tulikubaliana na rafiki yangu Frank Knows twende kujaribu kununua mzigo China, tulisubiri kipindi cha tiketi za offer na tukapata Ethiopian Airways, tulifanikiwa kufanya utafiti wa maana sana China na tukajilaumu tulikuwa wapi siku zote, Ndoto zangu nlianza kuziona zikikamilika licha ya kuwa China ilitakiwa uwe na hela nyingi na wote tulisafiri na pesa kidogo sana hazikutosha kununua mzigo.

Nilitafakari nifanye nini? hesabu zetu zilionesha kununua mzigo mdogo China ni kazi bure na hela itapotea, mwisho wa siku niliamka asubuhi nkamuita Frank nikamwambia “Nimeamua kukupa hela yangu yote ukifanikiwa utanishika mkono ukifeli tutakuwa tumejifunza kitu” alinishangaa sana, Alipojumlisha na yake jumla ikawa million kumi na mbili (12mil), Nlifanya hivyo kwa sababu zifuatazo;

Moja, Nilijua lazima mmoja wetu akubali kuwa na subira na mwingine atangulie (urafiki wetu hatukuwahi kuweka wivu na ubinafsi mbele)

Pili, Frank alikuwa na wateja wengi kuliko mm hivyo angezungusha hela haraka zaidi. (Ni vema kukubali ukweli)

Nilimuacha Frank akazungusha hela kwa muda kama wa miezi 6 na alikuwa akisafiri mara kwa mara, nlifurahi kumuona akifanikiwa na nilimsaidia sana kutafuta wateja na kumshauri, baada ya hapo alikuja akanipa 20,000,000/= (Cash) na tukaondoka wote tukaenda China kufunga mzigo. Nilifunga mzigo mzuri sana sababu Frank alipata experience kubwa na alikuwa ananionesha masoko mazuri bila kuona wivu.

Moral of the story (Jambo la Kujifunza) : Urafiki wenye wivu na ubinafsi hauna tofauti na kufuga ng’ombe dume wawili then utegemee kupata maziwa. 

Urafiki wenye Wivu na Ubinafsi hauna Faida. 

Yote haya aliandika Fred Vunjabei katika Ukurasa wake wa Instagram Mwaka 2021