JE, WAJUA
Mwaka wa 2014, Aires na miji mbalimbali hawatoisahau fainali ya Kombe la Dunia ambapo Argentina ilipoteza dhidi ya Ujerumani.Kibaya Zaidi, Gonzalo Higuain hakuweza kupata usingizi kwa makelele ya mashabiki wengi wa Argentina kwa kupoteza nafasi za wazi alizopokea kutoka kwa Lionel Messi. Messi aliibuka mchezaji bora lakini hakuwa na furaha kabisa.Miaka 8 baadae, Lionel Messi anakuwa mchezaji pekee aliebaki katika kikosi cha 2014 na siku ya Jumapili Desemba 18, atajaribu karata yake ya mwisho dhidi ya Wafaransa ambao ndio mabingwa watetezi. Je, Messi atafanikiwa kustaafu akiwa na medali ya Dhahabu ya kombe la Dunia?