MOVIE NA VICHEKESHO

THAMANI YA BINADAMU HAIDUMU MACHONI MWA WAJA!!

THAMANI YA BINADAMU HAIDUMU MACHONI MWA WAJA!!

Tujifunze kwa maisha ya mchezaji wa taifa la Ureno na Superstar wa dunia Cristiano Ronaldo (CR7).

Ronaldo amekuwa role Model wa vijana wengi wapenda soka duniani kwa miaka zaidi ya 12+ hata wale wasiopenda soka walimkubali sana.

Kwa ujumla dunia nzima ilimjua Ronaldo na kila mzazi alitamani mwanaye angekuwa kama Ronaldo. ##www.absalomfamily.com

CR7 kama binadamu wengine, sasa amechoka baada ya kazi ngumu aliyoifanya katika viwanja Mbali Mbali barani ulaya, kwa sasa akili yake inataka ila mwili hautaki.

Kwasababu hawapi mashabiki zake wanachohitaji, basi wamemgeuka ni mwendo wa kumtukana, kumuombea mabaya, kumzodoa, kumdharau na kuona siyo mtu tena wa maana kwenye soka.

Kundi kubwa la wanaosema CR7 hafai ni wale ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuvaa majezi yenye jina lake mgongoni na hata kujiita Ronaldo.

FUNZO:
Ishi maisha yako unayopendezwa nayo, jiwekee akiba yako maana kuna wakati utafika ambapo hao wanaokushangilia kwa sana watakuzomea kwa sauti kubwa zaidi!!!!

www.absalomfamily.com