MOVIE NA VICHEKESHO

MONEY HEIST

Money Heist: Korea ni adaptation ya Money Heist mnayoijua ?. Wengi mliosikiq ujio wa huu mzigo mlifikiri maybe kuna mambo yanaweza kua yamebadilika nadhani ni kushindwa kuelewa maana ya adaptation tu.

Mfano, The Good Doctor ilianza kutoka kwa Wakorea then baadae Hollywood waka adapt, almost S01 nzima ya Hollywood ni sawa kama ya Korea.

Kwa mimi ambae nilianza na Wakorea nilipoiona ya Hollywood niliona ni uduanzi tu, Naamini pia ambae atakua kaanza ya Hollywood akitazama ya Wakorea ataona ni uduanzi pia maana ni kama unarudia kitu kile kile kwa mazingira tofauti.

Kwanini kwenye filamu zinafanyika adaptation? Kwanza ni kuongeza faida zaidi mfano, Money Heist imewapa faida nzuri tu Netflix na tayari mzigo umemalizika, so hapo ndio huja tunaendelea vipi kupiga pesa zaidi kupitia franchise?

Njia mojawapo ni adaptation kwa masoko mengine ya filamu, then sometimes huwa tunaona zinaletwa Prequel na Sequal etc. So adaptation kama hii faida yake ni kuchukua pesa zaidi kwenye soko la Wakorea lakiniiā€¦

Hata ile Original iendelee kuuza maana kuna ambao hawajatazama kabisa, Lakini ni mafans wa Korea so wanaweza wakatazama alafu wakataka kuja kutazama zaidi Original version. So hapa ni ishu ya kibiashara zaidi.

Sitoshangaa kusikia baadae inakuja Squid Game kutoka Hollywood ?