FULL STORY|OMBA OMBA
Ilikuwa ni takribani miaka miwili imepita toka aonane na familia yake kwa sababu za ulinzi wa amani nchi mbali mbali duniani.
Sio tu mke..bali hata watoto wake walikuwa na furaha ya ajbu kumwona baba….Howard na samweli hawakubanduka kwa baba yao..wakimparamia paramia muda wote..
Ilikupata Muda mzuri na familia yake, Kamanda George alijadiliana na mkewe Jane kwamba waende mapumzikoni mbali na Nyumban.
Usiku ulikuwa mrefu sana kwa familia hii..wote walitamani kukuche waanze safari.
Mziki mzuri toka ndani ya speaker znye ubora ziliwaburudisha njiani…stori utani…vinywaji laini vilishushwa taratibuuu…furaha iliyoje ndani ya Mercedes benz new model.
Ghafla kukawa na mtikisiko mkubwa garini..vinywaji vikamwagika na wengine kujigonga..kutokana na brake ya ghafla…Mzee George alishindwa kujizuia kusimama ghafla baada ya kijana aliyemwona kwa mbali akichechemea kusogea barabarani ghafla akilia kwa sauti kubwa kuomba lift..
Kwa jinsi yule kijana alivyochoka..na kuchakaa..ambaye alisemani yatima na hana nauli alikuwa anaenda kijiji cha mbele akapate walau tiba…huruma ilimwingia Mzee George…
Mabishano makali yalizuka na familia yake…maana wazo la kutaka wa mbebe lilipingwa na wote kwa jinsi kijana alivyokuwa havutii..jasho..uchafu na hali nngumu alokuwa nayo…huku akiwa bado analia kuomba msaada..Mzee George akatumia mabavu kama baba kumchukua..
Ghafla gari likawa kimyaaa…howard na samweli wakiosogea mbali wasigusane nae…na wakiomba madirisha yafunguliwe..huku wakipuliza air fresher.
Masikini kijana wa watu hakuwa na la kusema…maana shida ilimbana..machoz yalilowansha shalti lake tu.
Baba kama ndio hivi tusingekuja huku..alisema howrd…kwa hasira Baba akageuka na kumkemea…na kumbe hilo lilikuwa kosa kubwa sana..
Aliporudisha macho barabarani …alistuka kuona lori kubwa sana limekaribia kabisa kugonga..na wote ndani ya gari walipiga kelele za kuomba Mungu…lakini haiukusaidia
Mlio mkubwa sana ulisikika..na gari ilibingilika mara tatu…ikaharibika kabisa..
Baada ya watu kuja kutoa msaada..Mzee George…ndiye aliyeumia vibaya na alikuwa akivuja damu sana..akakimbizwa hospitali…familia yake yote na yule waliyempa lift walipata majeraha kidogo… walimlilia baba yao…ambaye alikuwa hajitambui kabisa..
Baada ya madaktari kumpokea…na kumkimbiza ICU..waligundua amepoteza damu nyingi…na wakafanya vipimo haraka kujua hali ya damu yake kabla ya kumwongeza…
Daktari alirudi kwa mkewe, jane, akiwa amepigwa butwaa na kile alichokiona kwenye damu ya mzee george..
Akamwambia.Tumempoteza Mzee..tumempoteza..
Kwani vipi tuambiee…aliuliza Jane huku akiwa amekumbatiana na watoto wake ambao wamechafuka vumbi baada ya kugaragazwa kwenye ajali….babaa..babaaa…walilia
Muda wote huo ..yule mtoto yatima alikuwa amejikunyata kwa hofu na huzuni na upweke…moyoni aliumia kwa sababu huyu mzee alitaka kumsaidia na kwamba bila yeye ..asingegeuka na kupata ajali…
Daktari akamwonyesha majibu Jane….angalia..angaliaa…
Jane kaangalia na bado haukuelewa….Dr akamwambia soma hapa..akaona pameandikwa (0-)….Shemeji wenye damu hii hawazidi 5% tu duniani ..hatuna hii damu hatuna…tumempoteza
Dr sasa mbona hujatupima sisi ..tupimee…Dr akawaambia hakuna haja ya kujisumbua..damu hii ni adimu sana…
Kuwaridhisha akachukua vipmo..vya mama na watoto wake na akarudi machozi yanamtoka..hakuna ..
Dr akawaambia mbona mlikuwa wanne mmoja hajapima…wakasema hatuhusu huyo..tulimwokota njiani…na damu yake haiwez kuwa salama…anaumwa..
Dr alipomwangalia yule yatima…akaona kweli amedhoofu..akamwonea huruma akasema ngoja tumpeleke maabara tujue anatatizo gani asaidiwe..
Mungu wangu weee..Munguuu….Kelele kali zilisikika toka maabara.
Dr akaja kwa spidi kama amechanganyikiwa…anahema juu juu
huku akionyesha karatasi…0-, 0-,0-,0-…yule mtoto ni O- …
Haraka haraka yule mtoto yatima akafanyiwa utaratibu wa kutoa damu na kumwongeza Mzee george….
Mama na watoto wake wakilia na kumwomba msahama yule mtoto..Aligeuka lulu..Walimkumbatia..wakambusu…
Mzee george hatimaye akapona na Akam adopt na kuwa mwanae halali…Furaha ikarejea
NI MARA NGAPI TUMEWADHARAU WATU KWA MWONEKANO NA HALI ZAO…HUJUI NI NANI AMEBEBA FUNGUO ZA UZIMA WAKO,ZA MAFANIKIO YAKO.
YAWEZEKANA KWA HALI ULONAYO,UMASIKIN, UGONJWA,UNYONGE NA UDHAIFU WOWOTE..WATU WAMEKUDHARAU..NDUGU WAMEKUTENGA..IPO SIKU NA SAA UTAKUWA LULU..UTAKUWA DHAHABU.
TUHESHIMU NA KUJALI KILA ALIYEMBELE YETU….TUSIMLAZISHE MUNGU ATUPITISHE KWENYE MOTO ILI KUTUFUNDISHA
PENDA,JALI, HESHIMU BILA KUBAGUA Kanyaga Twende
HATUKUZALIWA NA NGUO..MAGARI..MALI..VYEO NK..TUMEVIKUTA NA TUTAVIACHA…TUVITUMIE KAMA NGAZI YA MAWASILIANO NA MUNGU…NA KAMWE VISIWE UKUTA .
©Absalomfamily2022