MOVIE NA VICHEKESHO

FULLY STORY|SUMU YA KUMUUA MUME

Binti alifika kwa mama yake kumlalamikia kuhusu ndoa yake. Malalamiko yake yalikuwa kama ifuatavyo: BINTI: Mama, mume wangu amenishinda. Ninataka kumua lakini nakosa ujasiri wa kufanya hivyo, unaweza kunisaidia tafadhali? MAMA: Ndiyo binti yangu, ninaweza. Lakini kuna tatizo dogo utatakiwa kulishughulikia kwanza. Itakubidi uanze kutengeneza mazingira na hali ya amani kati yako na mumeo ili kwamba watu wasikutilie shaka kwamba wewe ndiye umehusika na kifo chake. Utatakiwa kuwa mwema sana, mpole na umhudumie kwa moyo wote. Uwe romantic, uwe unamshukuru sana, uwe mwenye subira, na mnyenyekevu kwake. Mchukulie kama mwanao badala ya kumchukulia kama mkubwa mwenzio au raia wako… usiwe mbinafsi, uwe mnyoofu, msikilize sana, msafishe, mnawishe, usimsumbue au kumponda. Mwanangu, nina uhakika kwamba unaweza kuyafanya hayo, huna sababu ya kuutilia shaka uwezo wako. Kazi hiyo ianze leo jioni. Je, unaweza kufanya hivyo? BNTI: Ndiyo mama. MAMA: Sawa. Sasa chukua huu unga mweupe ambayo ni sumu itakayomuua. Kila siku unapomuandalia chakula weka kidogo kwenye chakula hicho, itakuwa inamuua taratibu. Baada ya siku 30, binti akarejesha majibu kwa mama yake. BINTI: Mama, kwa kweli sitaki tena kumuua mume wangu. Amekuwa romantic sana, amekuwa mbembezi na mwenye upendo mkubwa. Ninampenda, amebadilika na amekuwa laini tofauti na mwanzo. Nifanye nini kuzuia sumu ile isimuue? Nisaidie mama yangu, tafadhali. MAMA: Hahahahahaha BINTI: Kwa nini unacheka? Muda unakwenda, nataka kuokoa uhai wa mume wangu. MAMA: Hapana mwanangu! Huna sababu ya kuwa na wasiwasi. Nilikupa unga wa muhogo. Hatokufa. Ukweli ni kwamba, sumu ulikuwa nayo wewe. Unapostawisha chuki, kero na maudhi, vitu hivyo vinaua taratibu kuliko hata sumu, hivyo nililazimika kukushughulikia wewe kwanza badala ya mumeo. BINTI: Hmmmmmm. Ahsante mama’ngu kipenzi. DONDOO MUHIMU: ☛Itengeneze furaha yako na kuwafanya wanaokuzunguka kuwa na furaha. ☛Unapoanza kumpenda na kumthamini mumeo, mkeo, kaka yako, dada yako, mwanao, mama yako na baba yako, utayaona mambo mazuri na matamu kwao. ☛ Usisubiri mpaka mtu aumwe au afe ndo unaanza kumkubali, kumthamini na kumtukuza. ☛ Kabla hujaanza kulalamika, angalia kama tatizo halitokani na wewe. ☛Ishi kwa amani na kila mtu. Tuna uwezo wa kuona mazuri kwa wenzetu tukiwa na MTAZAMO CHANYA na iwapo hatutajipa sumu ya MTAZAMO HASI kwa kuyaona MABAYA yao tu tukaacha kuyaona mazuri yao pia..

www.absalomfamily.com

©Absalomfamily2022