FULL STORY|TUTAONANA MBINGUNI MPENZI
“Ta, ta ,ta” ilikuwa ni sauti ya mshale kuhesabu sekunde wa saa ya ukutani, yapata saa tisa usiku, ni ndani ya chumba kidogo, chumba pweke, Chumba kilichogubikwa na ukimya wa ajabu.
Ndani ya chumba kile kulikuwa vitu vilivyo hesabika, kigodolo kidogo kilicho chakaa kikiwa kimetandikwa chini katika sakafu, ndoo ndogo yenye maji ya kunywa, kamba ya katani iliyokuwa iking’inia ukutani, pamoja na begi dogo la nguo.
Mwanga mdogo ulitoka katika mshumaa uliokuwa ukikaribia kuishilizia uliweka nuru ndogo ndani ya chumba kile, Binti mmoja mwanamwali, mwenye sifa zote za kuitwa mrembo, alikuwa ameketi kitako juu ya kile kigodolo chakavu.
Kimakadilio alikuwa na umri kati ya miaka 21 ama 25, mweupe wa ngozi, sura iliyochongoka na kufanya mwenekano wa kisomali, macho makubwa yenye kurembua wakati wote, sanjari na kifua kilicho beba matiti yenye kusisimua mwili wa rijali yoyote.
Ajabu!…Binti yule alikuwa akilia, machozi mengi yalikuwa yakimiminika kama maji machoni mwake, mara kadhaa alitoa sauti ndogo ya kwikwi za kilio huku akipandisha kamasi kwa ndani.
Alisimama wima, taratibu akaliendea begi la nguo, akatoa kalamu na kalatasi, akarejea kwenye kigodo na kuketi tena.
Akapangusa machozi kwa viganja vyake, kisha akaanza kuandika ujumbe kwenye ile karatasi.
Ujumbe ule ulionza na neno ‘Tutaonana Mbinguni mpenzi’, ulisomeka hivi:
* Ilikuwa ni December 14 mwaka 2015. Ilikuwa ni Mara ya kwanza kuingia kwenye ulimwengu wa mahaba, kati yangu na mvulana mmoja aitwaye Reubeni Sabastian Maiga. Wakati huo nilikuwa na miaka 22 tu, nikiwa mwanafunzi wa chuo kimoja cha serikali huko mkoani Mara wilaya ya Bunda. Uhusiano wangu na mvulana huyo , ulikuwa umezingirwa na matarajio na ndoto nyingi maishani, kwangu Reuben alikuwa ni zaidi ya mpenzi. Nikiwa binti nisiyekuwa na wazazi wala ndugu yoyote nimjuye katika dunia, niliamini kijana huyo ndiye ndugu pekee maishani. Nilimpenda kwa moyo wangu wote, nikiamini ni baba wa watoto wangu wajao. Siku zilienda na miezi ikakatika, kama wasemavyo wahenga, kisicho riziki hakiliki, miezi kadhaa nikiwa kwenye penzi motomoto na mvulana huyo, mara nilikumbwa na maradhi ya ajabu. Maradhi hayo yaliniliza kitandani kwa miezi miwili, huku nikipata matibabu kwenye hosptali ya DDH ya pale wilayani Bunda. Kubwa lililonisibu, nilikuwa na uvimbe kwenye kwenye via vya uzazi,(Polycystic Ovarian Syndrome) (PCOS). nilitakiwa kufanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe ule. Hata hivyo changamoto ikaja kwenye gharama za matibabu. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuvurugika kwa dira ya maisha yangu. Pesa iliyohitajika kwa ajili ya matibabu ilikuwa siwezi kuimudu, Reuben akajitahidi kadri ya uwezo wake bado alishindwa kuipata shilingi laki tano kwa ajili ya matibabu. Hali yangu ikazidi kuwa mbaya siku hadi siku. “You have to use extra effort to save her, otherwise she will die, if the splitting will not take place within one week she is going to die”(Usipofanya jitihada za ziada huyu binti atakufa, na sipendi kukuficha, siyo zaidi ya wiki moja anaweza kufa kama asipofanyiwa upasuaji na uvimbe kuondolewa) Siku moja daktari alimwita Reeben na kumweleza. Kijana yule alifanya kila linalowezakana kutafuta pesa kwa ajili ya kuokoa maisha yangu… lakini wapi, shilingi laki tano alishindwa kabisa kuzipata. Hali yangu nayo ikazidi kuwa mbaya. Hatimaye Reubeni akafanya jambo moja ambalo binafsi naliita la kujitoa muhanga, kwa ajili yangu akafanya uvamizi katika duka la Tigo pesa na kufanya wizi wa pesa. Hata hivyo bahati haikuwa yake, wananachi walimkamata na kumshushia kipigo cha haja, jambo baya kuliko yote walimwagia mafuta ya petrol na kumchoma moto. Reubeni akafa akiwa anapigiania uhai wangu, akafa akiwa na maumivu makali, akafa akiwa na ndoto zake maishani. kila kitu kilizimika ghafla mithili ya kibatari kwenye upepo. Lilikuwa ni pigo baya maishani, Rubeni alizikwa nikiwa hoi kitandani, sikupata walau nafasi ya kuaga mwili wake, sikupata fursa ya kusema kwaheri, historia ya mwanaume niliyempenda ilishia hapo. Nikiwa hoi kitandani daktari alinieleza kuwa kidonda kilichopo ndani ya mwili wangu hakiwezi kupona tena, alisistiza kuwa hayo ni matokeo ya kukawia kupata matibabu. Akaniandikia vidonge vitakavyonisaidia kutuliza maumivu huku nikingoja mauti. Nikaruhusiwa na kurudi nyumbani. Sasa ni saa saba usiku, maumivu ni makali moyoni na mwilini mwangu, sioni haja ya kuendelea kuishi kwenye dunia ya mateso, najua baadhi ya watu watabeza maumuzi ninayokwenda kuayachukua. Moyo wangu umeridhia hilo, sina kitu muhimu katika maisha, niliipenda dunia lakini dunia haukunipenda. wasalam. Khadija Usi Abdallah. @@@@@@
Baada ya kumaliza kuandika barua ile, binti yule aliikunja vizuri na kuipachika kwenye kile kigodolo.
Akashusha pumzi ndefu huku kwikwi ya kilio ikiendelea kumtoka, kamasi nalo likawa linachungulia na kurudi kwa ndani.
Alitengeneza kitanzi katika kamba iliyokuwa ikining’inia darini, kisha akijivisha shingoni kamba ile na kupanda juu ya dari.
Ghafla alijiachia na kuanza kuni’ginia huku akitapatapa macho yamemtoka pomoni, dakika tatu badaye tayari msichana yule alikuwa maiti.
Historia ya binti yule ambaye pia ni yatima ikaishia hapo.
Mwisho USHAURI:
Una nguvu kubwa ya kuvumilia machungu huku ukiamini kwenye kesho iliyo njema. Hakuna mwenye juhudi aliyeshindwa mpaka mwisho. Mambo yatakuwa magumu mwanzoni na Katikati. Ugumu mwingine hukuandaa tu katika kubwa zuri lijalo. Ukiishia kati itadhihirisha hukukua kiasi cha kutosha kufanikiwa
wakati mwingine katika maisha shida na matatizo ni lazma ziwepo ili kuchochoea dhamira ya kufikia kilele.
©Absalomfamily2022